Translate

Saturday, August 31, 2013

WALIMU WAOMBA KUPUNGUZWA UMRI WA KUSTAAFU.

WAKIMU katika tarafa ya MATOMBO mkoani Morogoro wamependekeza katiba mpya itamke kupunguzwa kwa mda wa utumishi wa uma kazini kutoka miaka 60 hadi 50.


Monday, August 26, 2013

NIDHAMU YA MWANAFUNZI.

Nidhamu shuleni ni kitu cha muhimu sana kwa maendeleo ya mwanafunzi, mwanafunzi assiye kuwa na nidhamu basi taaluma yake huwa ndogo sana, mfano,kuna shule moja ya sekondari manispaa ya morogoro yenyewe ina waalimu wa masomo yote na waalimu huingia darasani kufundisha lakini cha ajabu matokeo ya kidato cha nne 2012 wameanza na division iv ambao ni wanafunzi 21 tu kati ya 110 wengine 89 wamepata ziro.

Nidhamu ya mwanafunzi hutengenezwa na mwanafunzi, wazazi, utawala wa shule na walimu kwa ujumla, kusipo kuwa na ushirikiano nidhamu ya mwanafunzi huyumba na kushuka kitaaluma pia.
Je nini kifanyike-je nikumzira mwanafunzi, kumrekebisha au kumwachia mkuu wa shule peke yake?

Sunday, August 25, 2013

MIMBA MASHULENI

Kama kweli tunahitaji kupunguza mimba mashuleni, basi somo la uzazi lifundishe kwa undani toka mwanafunzi akiwa darasa la tano.


WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI WANAPATIKANA HAPA.

Kama unashida na walimu wa masomo ya sayansi shuleni kwako ( Chemistry, Biology, Mathematics, Geography na Computer) wasiliana na mimi kwa namba 0753285271 utampata.

MWALIMU WA KIZAZI KIPYA aka DOTIKOM.


Friday, August 23, 2013

Shule iliyopo manispaa ya Morogoro haina choo cha walimu.


Shule hii (TUBUYU) iliyopo manispaa ya Morogoro haina choo cha walimu.
Walimu hujisaidia katika choo ( choo hicho hakina hata mlango) kilichopo karibu na nyumba ya mkuu wa shule ambapo mwalimu huhitajika kutembea umbari mrefu hadi kufika chooni..............je kama mwalim kabanwa na tumbo itakuwaje?
Naomba mchango wenu wa kifedha ili kusaidia kujenga choo cha walimu.